Kajala na Wema Sepetu Bado Paka na Panya, Wakwepana laivu Kwenye Sherehe

WASANII wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja zamani walikuwa marafiki wa kupika na kupakua kabla ya kugeuka kama paka na chui, juzikati kwenye sherehe ya arobaini ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema walikwepana na kushindwa kusalimiana.

Katika tukio hilo, Kajala ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika kwenye sherehe hiyo ulipofika muda wa kuitambulisha kamati ya maandalizi mbele ya mashabiki, Kajala alijitokeza mbele pamoja na wanakamati wenzake lakini baada ya muda Wema aliingia kwenye sherehe hiyo.

Sherehe ikiwa imenoga na wageni walipozidi kuongezeka, Zamaradi aliwaomba wanakamati watoke tena mbele wajitambulishe tena ambapo muda huu wanakamati walijimwaya tena mbele ya mashabiki akiwemo Wema lakini Kajala hakutokea kama ilivyokuwa awali.

Jambo lingine lililoonesha wawili hao kukwepana lilijidhihirisha kwa jinsi walivyokaa ambapo wanakamati wote ambao waliovaa sare walikaa kwenye meza maalum lakini Kajala alikwenda kukaa upande mwingine akiwa na Johari na Shamsa Ford ambaye naye alikuwa amevaa sare ya kamati.

Na: Richard Bukos

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad