Sikia.... BAKI NA HELA ZAKO
Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Lete Raha vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.
Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.
Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je?
Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition.
Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Juzi tu Landmark Hotel ikawa Hostel.
Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo.
Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.
Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?
Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa.
If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.