Kangi Awavaa Waliokula Mabilioni ya Vitambulisho


Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amewataka wamiliki wa kampuni saba zilizopewa zabuni ya ukandarasi wa mfumo wa utambuzi wa watu katika zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kuripoti ofisini kwake siku ya Agosti 3, 2018 na pesa walizolipwa.


Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 25, 2018 katika mkutano wake wa waandishi wa habari jijini Dodoma, ambapo ameyataka makampuni hayo kufika ofisini kwake na kiasi chote cha fedha walizolipwa  ili zirejeshwe katika mfuko wa Serikali.

“Miongoni mwa kampuni hizo ni Gotham international Ltd (2.8bilioni), Iris Corporation Berhard (22.9bilioni), Gwiholoto impex ltd (Sh 946.4milioni), Skyes Travel Agent (5.9milioni), Dk Shija Paulo Rimoy (Sh 27milioni) ,Aste Insurance (sh 1.2bilioni) na BMTL (Sh569.1milioni)”, amesema Lugola.

Aidha Waziri Lugola amemtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kuripoti ofisini kwake siku hiyo ili akatoe maelezo ya ufisadi huo wa Shilingi bilioni 28.5.

Julai 21, katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es salaam, Waziri Lugola  alimuagiza aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) afike ofisini kwake Julai 25 ambayo ni leo akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya taifa, jambo ambalo limeshindikana kutokana na waziri kuwasili Dodoma leo mchana akitokea Arusha alikokuwa katika ziara yake ya kikazi aliyoikamilisha asubuhi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad