Kangi Lugola Atinga Ofisi Ndogo Wizara ya Mambo ya Ndani Kukabidhiwa Ofisi

Kangi Lugola  Atinga Ofisi Ndogo Wizara ya Mambo ya Ndani Kukabidhiwa Ofisi
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasili katika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kukabidhiwa ofisi baada ya kuapishwa.

Lugola ambaye ni mbunge wa Mwibara aliapishwa jana Julai 2, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam akichukua nafasi ya Dk Mwigulu Nchemba ambaye ameachwa kwenye baraza la mawaziri la Rais John Magufuli.

Waziri Lugola amepokewa ofisini leo Julai 3, 2018 saa 5:20 na viongozi na watumishi wa wizara hiyo.

Baada ya kushuka ndani ya gari, Lugola alisalimiana kwa kukumbatiana na Masauni. Pia, alisalimiana na katibu mkuu na manaibu wake.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad