Ndoa ya Zabibu Kiba na Abdi Banda Yanukia


KAPO’ inayoonekana kuwavutia wengi mtandaoni ya mwanasoka Abdi Banda na dada wa staa mkubwa wa muziki Bongo, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’, Zabibu Kiba imekuwa gumzo baada kuonekana dalili kuwa, wawili hao wataoana mwezi Agosti, 2018.



Gumzo hilo limekuja baada ya Banda anayeichezea Timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini kumposti mchumba wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha akaandika hivi; “Maamuzi sahihi, Get ready AUGUST. Unapenda tarehe gani?



Kufuatia swali hilo, wadau wengi waliamini Banda anaizungumzia ndoa yao hivyo wengi wakamshauri tarehe ya kufanya tukio hilo huku wengine wakiishia kuwaombea kila la heri ndoto yao ya kuwa mwili mmoja itimie.



“Mimi siku yoyote mtakayofunga ndoa ni poa ila iwe haraka jamani, naipenda sana kapo yenu,” aliandika mdau mmoja aliyejiita Kissbway.

Zabibu alipotafutwa kuzungumzia tarehe ya ndoa yake alisema, bado hawajapanga ila watu wanaweza kuendelea kupendekeza tu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad