Karen Aelezea Baba Yake Hakutaka Afanye Muziki, Ataja Mchango wa Jay Dee Kwake.

Msanii chipukizi wa bongo malkia karen amefunguka na kusema kuwa katika kufanya kazi ya muziki alipata upinzani mkubwa sana hapo mwanzo kutoka kwa wazazi wote wawili.karen ambae ni mtoto wa captain g habash anasema kuwa baba yake mara nyingi alikuwa akiogopa sana kuhusu maadili hasa kukaa vizuri sana mbele za watu.

Baraka zote zipo kutoka kwa wazazi wote wawili,mwanzoni ilikuwa ngumu sana kwa wote wawili na pia kwa uapnde wa baba ni kwamba kwa sababu yeye tayari ni nguli katika tasnia ya muziki kwaio alikuwa  anajua, kikubwa alikuwa  anakazania maadili tu,

Lakini pia Karen anakiri kuwa moja ya wat waliochangia sana kufika katika muziki na kufanikiwa ni mama yake mdogo Jay Dee ( ambae alikuwa akiishi na baba yake kwa ndoa) kutokana na kukaa nae vizuri lakini pia alikuwa akimlea vizuri na kumpa ushawishi mkubwa wa kufanya muziki.

Nilishawahi kukaa nae na alinilea vizuri sana hasa katika muziki,Kwakweli alini-inpire sana na katika nyimbo ninazozipenda ni ule wa faraja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad