Kenya Yapiga Marufuku Matumizi ya Dawa ya HIV

Kenya Yapiga Marufuku Matumizi ya Dawa ya HIV
Wizara ya Afya nchini Kenya imezionya kaunti nchini humo kusitisha kuwapatia wagonjwa dawa za HIV zinazosababisha kasoro miongoni mwa watoto walio tumboni.

Kupitia Mkurugenzi wa huduma za matibabu nchini humo Jackson Kioko, wizara hiyo imewaagiza Wakurugenzi wa afya katika kaunti hizo kuhakikisha kuwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha ambao walikuwa wakitumia dawa aina ya kwanza ya Dolutegravir (DTG), waendelee kutumia dawa hiyo hadi watakapomaliza kunyonyesha.

Lakini akina mama wajawazito walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 49 ambao wamekuwa wakitumia dawa hiyo wanapaswa kupewa matibabu ya kwanza ya Efavirenz.

Mapigano kati ya vikosi vya Uganda na DRC katika ziwa Edward
Katika taarifa kwa wakurugenzi hao Dkt. Kioko alisema kuwa dawa hiyo iliozinduliwa nchini Kenya mwaka uliopita haifai kutumiwa na wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha kutokana na data chache za usalama wake zilizopo.

Pia ameongezea kwamba kulingana na taarifa ya mwaka 2017, watu wazima wanaotumia dawa ya kwanza ya ARV wataanza kutumia DTG.

Hatahivyo mwenyekiti wa bodi ya madaktari nchini Kenya tawi la magharibi Dkt Anthony Akoto amesema kuwa wizara ya afya inapaswa kutoa sababu za hatua hiyo zikiandamana na ushahidi.

Akizungumza na BBC, Dkt Akoto anasema kuwa kufikia sasa hakuna ushahidi wowote kwamba dawa hiyo ina madhara na akivitaka vitengo muhimu vya serikali katika wizara ya Afya kama vile Kemri, Shirika linalosimamia udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi NASCOP, na shirika la ubora wa bidhaa KBS kutoa ushahidi unaothibitisha dawa hiyo haifai kupewa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha.Kenya Kusitisha
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad