Mwanamitindo na mke wa Star Kanye West, Kim Kardashian amechukua hatua tofauti katika maisha yake ya ustar na kuamua kuwa mtetezi wa mabadiliko ya sheria “Advocate for Prison Reform” katika moja ya gereza lenye wafungwa wengi Duniani.
Baada ya kuweka historia ya kukutana na Rais Donald Trump kwaajli ya mazungumzo ya kumuachia mfungwa kwa jina la ‘Alice Marie Johnson (miaka 63)’ ambae alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya uhalifu unaohusiana na madawa ya kulevya mnamo mwaka 1997.
Kim Kardashian anataka kuweka historia nyingine baada ya kutembelea gereza la wafungwa wa kike huko Corona, California, ambapo alifanya ziara na kuongea na wafungwa kuhusu mipango na mustakabali wa maisha yao baada ya kifungo.
Chombo kimoja cha habari kutoka nchini Marekani kimeripoti kuwa Mwanadada Kim Kardashian ameweka headlines baada ya kuwaambia wanasheria wake waisimamie kesi ya mwanamke mmoja aitwae ‘Cyntoia Brown’, Mwaka 2017 mahakama ilimhukumu ‘Cyntoia Brown’ kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanaume aliyembaka.
Kim Kardashian alitweet maneno haya “ The System has failed. Its heart breaking to see a young girl sex trafficked and raped then when she fights back she is jailed for life! We have to do better & do what’s right. I’ve called my attorneys to see whats can be done to fix this. #FreeCyntoiaBrown”