Kimenuka Yanga Wachezaji Wagomea Mazoezi

Kimenuka Yanga Wachezaji Wagomea Mazoezi
WACHEZAJI wote wa Yanga unaowajua wewe ambao usajili wao upo CAF jana Ijumaa waligoma kufanya mazoezi huku Kocha Mwinyi Zahera akiwasihi viongozi wawaambie mashabiki wa timu hiyo ukweli.

Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kur­asini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawa­jui.



Wachezaji wote waliocheza mechi ya Gor Mahia hakuna hata mmoja aliyeonekana mazoezini na Zahera hakuwa na taarifa yoyote lakini Cham­pioni limejiridhisha kwamba wameambizana kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi mitatu na kushinikiza pia mashabiki wajitokeze kuokoa jahazi.



Yanga Jumatano ya wiki hii ilipigwa mabao 4-0 na Gorma­hia kwenye mechi ya Shirikisho na timu hizo zitarudiana Dar es Salaam Ijumaa ijayo saa 1.00 usiku.


Zahera ambaye si mzun­gumzaji sana jana Ijumaa alia­mua kufunguka mpaka tone la mwisho kwa viongozi akiwam­bia wawaambie mashabiki na wanachama ukweli kuinusuru timu hiyo na kumrahisishia kazi yake.



Zahera alipofika uwanjani hapo alikuta kuna wachezaji watano pekee ambao ni; Deus

Kaseke, Heritier Makambo, Mrisho Ngasa, Emeka Emerun na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ hali iliyomfanya asitishe mazoezi hayo mpaka leo Juma­mosi.



“Kiukweli uongozi wangu unanipa wakati mgumu sana wa kuifundisha hii timu, kwani ni vigumu sana kwa sasa kutege­mea kupata matokeo kwenye mchezo ujao wa marudiano dhi­di ya Gor Mahia kwa staili hii ya wachezaji kuwa na kasumba ya kukimbia mazoezi kila kukicha.


“Naomba viongozi wangu waache kuficha ukweli badala yake wajitokeze hadharani wawaambie mashabiki kuwa timu inamatatizo ya kifedha ili kama kuna ambaye ataguswa na kuona kuna haja ya kuichangia afanye hivyo ili wanipun­guzie mzigo wa kugombana na wachezaji kama leo ambapo tulielewana tuanze mazoezi lakini wote waliokuwa safarini hawajatokea,”alisema Kocha huyo raia wa Ufaransa.



“Nimeshindwa kufanya maz­oezi leo kutokana na kukutana na wachezaji watano tu na hawa wote hakuna hata mmoja am­baye naweza kumtumia kwenye mechi ijayo kutokana na wote hao hakuna aliye na leseni ya Caf.



“Kama watagoma zaidi ya siku tatu zijazo maana yake ni kwamba hata uwezekano wa kucheza mechi ijayo utakuwa mgumu kwetu lakini hata hivyo kupata matokeo pia itakuwa ni hadithi tu,” alisema Zahera am­baye msaidizi wake aliyetua hivi karibuni ameshaingia mitini.



Alipotafutwa Kaimu Mwenyeki wa Yanga, Clement Sanga alise­ma: “Kwa sasa nipo nje ya ofisi siwezi kuzungumza lolote mpaka nitakaporejea kesho (leo).”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad