Kiongozi wa Mbio za Mwenge Agoma Kuzindua Zahanati Mbele ya DC Hapi

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Agoma Kuzindua Zahanati Mbele ya DC Hapi
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni DSM, Ally Hapi amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Wilaya ya Kigamboni na kushiriki uzinduzi wa miradi mbalimbali ndani ya Wilaya yake.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho amegoma kuzindua jengo la Zahanati ya Mkoroshini iliopo Msasani kutokana na gharama zilizotajwa kutumika kwa ujenzi wa jengo hilo kuwa Milioni 406 ambazo haziendani na kiwango cha jengo hilo.

Kabeho amewataka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati suala hilo kwa undani ili kuweza kubaini wizi uliofanyika katika jengo hilo.

“Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 haujaridhika na gharama za ujenzi wa jengo hili hivyo sitaweka jiwe la msingi, taratibu zote zikifanyika nikajiridhisha nitaweka jiwe la msingi kwa utaratibu” amesema Kabeho
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad