Kiongozi wa Upinzani Nchini Zimbabwe "Jina la Zimbabwe Limelaaniwa Libadirishwe''

Kiongozi wa Upinzani Nchini Zimbabwe "Jina la Zimbabwe Limelaaniwa Libadirishwe'
Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa ameapa kuwa atalibadilisha jina la nchi hiyo na kuwa "Great Zimbabwe" akieleza kuwa jina la sasa la nchi hiyo lina 'laana', kwa mujibu wa mtandao wa New Zimbabwe.

"Zimbabwe haiwezi kusalia kuwa Zimbabwe, kwasababu imegeuzwa kuwa gofu la Zimbabwe," Chamisa aliwaambia maelfu ya wafuasi katika mkutano wa kisiasa mashariki mwa mji wa Mutare.

"Jina la Zimbabwe limelaaniwa kama mnavyoona timu yetu ya taifa ya soka inashindwa kila saa katika mechi - kriketi tunashindwa, voliboli daima inashindwa," aliongeza kusema.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 40 ananuia kuwa rais katika uchaguzi mwishoni mwa mwei huu Julai 30 - uchaguzi ulio wa kwanza baada ya kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kuondoka madarakani.
.

Zimbabwe ilijulikana kama Rhodesia kusini kati ya mwaka 1898-1964, ambalo ni jina la Mkoloni wa Uingereza Cecil Rhodes. Mapema 1960, however, raia wenye utaifa walianza kuliita taifa hilo Zimbabwe. Jina linalotokan ana maneno mawili "dzimba" na "dzamabwe" (yenye maana ya nyumba ya mawe) kwa lugha ya Shona inayozungumzwa pakubwa hivi leo Zimbabwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad