Kiungo wa JKU Asaini Miaka Mitatu Singida United

Kiungo wa JKU Asaini Miaka Mitatu Singida United
Klabu ya Singida United imefanikiwa kuinasa saini ya  mchezaji Feisal Salum Abdalah “FEI TOTO” kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Katika kikao cha pamoja cha Uongozi wa JKU na Singida United, wameshakubaliana gharama za kufidia mkataba (transfer fee) wa miaka miwili ambayo mchezaji huyo alibakiza kuitumikia JKU.

index
Toto ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga amefikia makubaliano na uongozi wa Singida kwa kusaini kandarasi hiyo na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha walima alizeti hao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hii ni mwendelezo wa kukisuka kikosi cha Singida United kilichopo chini ya kocha Hemedi Selemani Morocco ambaye amechukua mikoba kutoka kwa Mholanzi Hans Van Der Pluijm aliyetimkia Azam FC
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad