Kuhusu Kufariki Kwa Mchezaji wa Yanga Kamusoko


Mapema leo katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa zilizodai kuwa kiungo msambuliaji wa klabu ya Yanga, mzimbabwe Thabani Kamusoko amefariki kutokana na ajali iliyohusisha gari aina ya Noah.

www.eatv.tv iliutafuta uongozi wa Yanga, ambapo kupitia Afisa habari wake Dismas Ten amekanusha taarifa na kudai kuwa ni za uzushi na tayari wamesharipoti kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake na kusema kuwa mchezaji wao yuko salama akiwa tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

“Taarifa hii ni uzushi, mtu huyu amekuwa akifanya hivi mara nyingi kuwazushia watu mbalimbali vifo, alifanya hivyo kwa baadhi ya wachezaji pia kama vile Mrisho Ngasa na Hassan Kessy na vingozi mbalimbali wa Serikali na leo ameandika hivi kwa Kamusoko”, amesema Ten.

Yanga itakuwa dimbani leo ikimenyana na Gor Mahia ya Kenya, katika mchezo wa wamarejeano kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad