Kujiuzulu Kwa Waitara na Jokate Kupewa Ukuu wa Wilaya


Je, ni kweli Waitara ameondoka Chadema kisa alizuiwa kugombea uenyekiti? Hii ni mpya. Ila kama Chadema wanaweza kumharasi mwanachama wao anayetaka kugombea uenyekiti, huo ni utoto, ni utovu wa demokrasia.

Angeachwa tu agombee halafu tuone kama Chadema wangeweza kumwondoa Mbowe ili Waitara aongoze chama chao. Kweli Mbowe abadilishwe kwa Waitara? Kwa maoni yangu Waitara hatoshi hata uenyekiti wa Shilawadu, itawezekana vipi uenyekiti Chadema?

KUHUSU JOKATE

Tanzania hakuna sheria yenye kumdhibiti Rais kufanya uteuzi kwenye ofisi za umma. Hivyo, humteua amtakaye kwa pendezo lake. Nini Jokate, angetaka hata Gigy Money angeweza kupewa ukuu wa mkoa.

Pongezi kwa Jokate na wote walioteuliwa ukuu wa wilaya, mkoa na ukatibu wa wizara. Wajibu mkuu kwa walioteuliwa ni kufanya kazi kwa bidii, wakifuata sheria na utu ili kumlindia hadhi aliyewateua. Wakiboronga, wanaobeza uteuzi hivi sasa wataongezewa cha kuongea.

Tafadhalini; msiingie ofisini kwa sifa na mbwembwe. Uongozi ni kivuli cha mpito, maisha ni safari ndefu. Hakikisheni mnatunza pumzi ili ziwafae safarini baada ya vijiti mlivyopokea kupokelewa na wengine.

Ndimi Luqman MALOTO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad