Kume Lulu Diva Kahamisha Kambi kwa Bill Nass na Si Rich Mavoko Tena

Kume Lulu Diva Kahamisha Kambi kwa Bill Nass na Si Rich Mavoko Tena
HITMAKER wa Ngoma ya Ona, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kutoka kimapenzi na msanii mwenzake, William Lyimo ‘Bill Nas’. Kwa mujibu wa ‘source’ wetu, wawili hao wamekuwa karibu kila kona na wala hawaoni aibu kujibebisha hadharani.

“Walianza kama masihara, tukajua labda Rich Mavoko ndiyo anakaa kwa Lulu kumbe ni Bill Nas bwana, juzi walikuwa tena pamoja wakielekea mkoani sijui mkoa gani lakini picha zao za kujibebisha zinamaanisha,” kilisema chanzo.Risasi Vibes halikuacha ishu hiyo iende ‘plain’ , lilimtafuta Lulu na baada ya kupatikana aliwaka;

“Hivi jamani mtu kuongozana na mwanaume ndiyo kutembea naye? Mbona mnataka kuniharibia kwa mtu wangu niliyekuwa naye?“Bill Nas ni mshikaji   wangu wa kawaida tu, juzi (Jumamosi iliyopita) tuliandaliwa shoo ya pamoja huko Iringa, tukiwa njiani tulikuwa tukipiga mapicha picha kama mtu na rafiki yake, nashangaa watu wanageu-zageuza maneno.”
Chanzo: Global Publishers

Top Post Ad

Below Post Ad