Kuna Siri Gani Kwenye Maji ya Kuoshea Maiti Yanapochanganywa Kwenye Chakula?


Ni mara nyingi nmekuwa nikisikia haya maji kutumika sana kwnye shughuli za kishirikina. Mfano kutumika kwenye shughuli za mama ntilie wakichanganya na msosi nasikia unakuwa mtamu sana ndo pale unakuta mazingira ya upishi na jinsi chakula kinavyoandaliwa unakuta hayaridhishi kabisa ila unakuta watu wanafurika muda wote na si ajabu unakuta mtu anafunga safari kutoka mbagara anaenda kula lunch ubungo!!! Ukimuuliza atakwambia msosi wa mama flani ni mtamu sana. Sasa nasikia ule msosi wakati wa upishi ukichanganywa na maji ya kuoshea maiti unakuwa mtamu sana na ndio silaha kubwa ya biashara wanayoitumia mama ntilie walio wengi.

Kuna mchawi mmoja niliwahi kumsikia mahali kwamba wakati walipokuwa wanaenda kumchukua mtu kwenye nyumba yake kwanza lazma waoge maji ya maiti ndo safari yao inaanza halafu wakifika kwenye nyumba wanayamwaga hayo maji kwenye pande nne za paa la bati alafu wakifanikiwa kuingia wanampaka alokusudiwa kuchukuliwa hayo maji kuanzia miguuni hadi utosini huyo mtu analala anakuwa kama anaota then wanambeba.

Duniani kuna mengi haya maji ya kuoshea maiti katika ulimwengu wa roho yana kazi kubwa sana !

Cc @ Mshana jr

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad