Kuondoka Kwa Mbunge wa Monduli CHADEMA ni Dalili ya Lowassa Kuachana na Siasa?

Tukio la Mbunge wa Monduli kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM limeanza kutoa picha halisi kuhusu hatma ya Lowassa ndani ya CHADEMA na katika siasa nchini.

Katika watu ambao walikuwa karibu sana na Edward Lowassa kisiasa wakati akiwa CCM na CHADEMA mmojawapo ni Julius Kalanga Laizer ambaye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia CHADEMA.

Julius Kalanga Laizer alikuwa ni mmoja wa watu ambao kama utataka kuonana na Lowassa wakati akiwa Mbunge lazima upitie kwake. Kwa maneno mengine alikuwa ni gatekeeper au kiunganishi cha Lowassa.

Mtu yeyote aliyetaka kugombea udiwani katika Jimbo la Monduli ilikuwa lazima kwanza akubaliwe na Julius Laizer akishirikiana na Isack Joseph na pia Paulo Kiteleki. Ikumbukwe kuwa bila ridhaa ya Lowassa kama unataka uongozi katika Jimbo la Monduli utakuwa unapoteza muda wako.

Lowassa baada ya kuachia Jimbo la Monduli aliamua kumkabidhi kijana wake Julius Kalanga Laizer ambaye alihama naye kutoka CCM na kujiunga CHADEMA.

Kwa sasa Julius Laizer ameamua kurudi CCM na kwa maana hii kuna uwezekano mkubwa Lowassa ameishawaeleza vijana wake kama Laizer kuhusu hatma yake kisiasa ndani ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa madiwani zaidi ya 7 kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Monduli wamejivua uanachama na kuhamia CCM.

Yajayo ndani ya CHADEMA yanafurahisha na kufikirisha!

Hii ndio faida ya mafuriko ya Edward Lowassa ambayo yako mbioni ‘’kuisomba’’ tena CHADEMA!

Swali la Dkt. Slaa bado VALID! Lowassa is an asset or a liability to the opposition party?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad