Kutana na Jamaa wa Kenya Anayetaka Kumuoa Bintiye Barack Obama Maasai Moran

Jamaa mmoja wa Maasai aliyejitokeza mnamo 2015 na kudai kuwa anataka kumuoa mwanawe Barack Obama ameonekana kutopoteza matumaini huku akijitokeza mara nyingine.

Jeff Ole Kishai alieleza kuwa yuko tayari kukesha mjini Nairobi kwa mara nyingine huku Obama akiwasli Kenya Jumatano, 27 Juni.

 Jeff Ole Kishai ameeleza kuwa atafanya kila awezalo kumuoa bintiye Obama.

Ili kumshawishi Malia, mwanawe Obama, Kishai ameeleza kuwa ameandaa ng’ombe 1,000 kama mahari.

Kuthibitisha mapenzi yake zaidi, jamaa huyo aliamua kutengeneza fulana yenye picha ya Malia atakayovalia akimsubiri babaye mwanadada huyo. 

‘’ Wakati ule mwingine, nilikuwana ng’ombe 500, niko tayari kuongeza 500. Nitalala Nairobi. Kuna reli hapa kuwasafirisha ngombe hawa hadi Nairobi,'' alisema Mamaye Jeff alieleza kuwa atafurahi mno iwapo mwanadada huyo atamkubali mwanawe.

 ‘’ Tutafurahi akija hapa Suswa. Tunatumahi Jeff atakutana naye ili waishi kama familia,’’ mamaye alisema.

Obama atatua Kenya Julai, 16, 2018 kwa ziara ya siku moja kabla kusafiri hadi Afrika Kusini Kama ilivyoripotiwa 

Top Post Ad

Below Post Ad