Akiwa na umri wa miaka 20 tu mwanadada mdogo kutoka kwenye familia ya Kardashian, Kylie Jenner, ametajwa Jumatano hii na jarida la Forbes kama binti mdogo bilionea wa America.
Jenner ambaye alijifungua binti aitwae, Stormi mwezi Februari, alianzisha vipodozi vya Kylie miaka miwili iliyopita na kampuni hiyo tayari imeuza zaidi ya $ 630 milioni kwa mujibu wa jarida moja la mitindo nchini humo.
Forbes wameitafsiri kampuni yake hiyo ina thamani ya $ 800,000,000 huku jarida hilo likidai huwenda thamani ya utajiri wake umeongezeka maradufu mpaka kufikia $ 900,000,000.
Mrembo huyo anamiliki asilimia 100 ya kampuni hiyo, ambayo ilianza na mtaji wa $ 29 kwa kuwa na seti ndogo za “lipstick” pamoja na bidhaa nyingine ndogo ndogo za urembo.
Kwa sasa binti huyo ndio tajiri mdogo zaidi kwa mujibu wa jarida la Forbes kwa wanawake tajiri zaidi ya Marekani, na ameweza kuwa tayari mdogo zaidi duniani na kumpiku Mark Zuckerberg, ambaye ambaye utajiri wake ulikuwa kwa kasi zaidi akiwa na umri wa miaka 23.
“Asante @Forbes kwa makala hii na kutambuliwa .. Nimebariki sana kufanya kile ninachokipenda kila siku,” alieleza Jenner.
Mafanikio yake yamehusishwa na umaarufu wake na uwezo wa kuimarisha vyombo vya habari vya kijamii. Ana wafuasi zaidi ya milioni 110 kwenye Instagram, milioni 25.6 kwenye Twitter na milioni 16.4 kufuata kampuni yake moja kwa moja.
Forbes alisema kampuni hiyo ina wafanyakazi saba tu wa muda wote na watano wa muda, pamoja na viwanda.
“As ultralight startups go, Jenner’s operation is essentially air. And because of those minuscule overhead and marketing costs, the profits are outsize and go right into Jenner’s pocket,” Forbes wrote.
Jenner ni binti mdogo kabisa wa Kris na Caitlyn, aliyekuwa na medali ya dhahabu wa Olimpiki Bruce. Dada yake ni supermodel Kendall. Na ndugu zake wengine ni Kim, Kourtney, pamoja na Khloe Kardashian.