Mimi ni mwanaume wa miaka kadhaa..Kilichonipelekea kuleta hii mada ni kwamba kila mwanamke ninayeamua kuwa nae ananipa majukumu mengi hata kabla sijamtamkia kwamba nimeamua kuwa nitamuoa, sikatai kwamba kumsaidia mpenzi wako ni jukumu ambalo haliepukiki lakini msaada unaotolewa usiwe ndo kigezo cha uwepo wa mapenzi yetu, kwa kipindi kirefu nimevumilia hili toka kwa wanawake kadhaa lakini sasa naona kama naelekea kushindwa, mimi binafsi najihisi kama nina mkosi vile kwa heshima yako naomba waeleze wasichana/wanawake kwamba wakati mwingine sisi wanaume tunakuwa na nia kabisa ya kuanzisha uhusiano imara wenye uwezo wa kuzaa ndoa,
Wanaume wengi unakimbizwa na "Mizinga" yao ya kila siku.katika mapenzi kuna kusaidiana, ila naona kama wenzetu wanawake wameona msaada pekee wa kupewa ni pesa, au wao pekee ndo wanastahili msaada,Wanawake wengi huwa wanaharibu uhusiano bila kujua, hakuna asiyekubali kwamba kusaidiana katika mahusiano ni jambo jema linalokubalika, lakini sasa imzidi jamani, si kila siku mtu unakuwa na pesa ya kukupa na pia ikumbukwe kwamba suala la kusaidiana katika mahusiano si la upande mmoja sote twawajibika kusaidiana, wanawake wengi baada ya kuwa katika mahusiano huamini kupata mtatuzi wa shida zake zote.
Mwanaume mwenye nia ya kweli na wewe akianza kukuona unaanza kumgeuza kitega uchumi, taratibu huanza kuzua visingizio vya kutoonana na wewe mwishowe anaishia zake.
Kitu kingine ambacho wanawake hawajui, si kila tatizo unampelekea mpenzi wako, mengine peleka kwa ndugu zako, hivi kila siku mnapotuomba pesa mwafikiri twazitoa wapi?
Sio wote wauza sembe, wanawake wengine wana kipato zaidi ya wanaume lakini bado hata kile kidogo tukipatacho mwataka, wewe kila kitu pesa, kwani mimi ndo nazitengeneza? hata kama unahisi ninazo nyingi, basi unadhani zote ni kwa ajili yako?
Hata mimi nina familia ya wazazi, wadogo zangu nk, nahitaji kuwahudumia, Tuhurumiane jamani, True love means give and take, twawapenda sana wake/wapenzi wetu lakini msitugeuze gari la mshahara
Najua tabia hii si kwa wanawake wote, lakini asilimia kubwa ndo hao, naomba kupitia blog hii tujaribu kuwekana sawa,kwa wale ambao wana tabia hizi na mnawajua, waelezeni,mnatuumiza, na ndiyo maana hatuishi kusikia vituko vya kina kaka kuwaachia bili wanawake katika sehemu za starehe,kujifanya wanaenda msalani,kumbe anakimbia kukwepa aibu,kwa maana hela ya kulipa hana