Lugola Amgeukia IGP Sirro Ampa Siku 14 Kujieleza

Lugola Amgeukia  IGP Sirro Ampa Siku 14  Kujieleza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mh. Kangi Lugola, ametoa muda wa siku 14 kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro kufika ofisini kwake kumueleza mikakati ya kuwawezesha Watanzania kufanya kazi kwa saa 24 ikiwa ni pamoja na kuzuia matishio ya mabasi kutembea nyakati za usiku.

Waziri Lugola ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuongea na Askari wa Kikosi hicho na wale wanaohudumia katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Wakati  akitoa agizo hilo, Mhe. Lugola amesema kuwa ili kufikia Uchumi wa kati Watanzania wanatakiwa kufanya kazi za kiuchumi kwa masaa 24 hivyo IGP anapaswa kumhakikishia mikakati ya jeshi lake katika ushiriki wao wa kuwapatia  watanzania usalama kwa muda wotewakifanya shughuli hizo za kiuchumi.

"Nataka IGP aje aniambie kwamba je, jeshi la polisi limesalimu amri kwa majambazi ndiyo maana mabasi hayatembei usiku, lakini biashara mbalimbali ikifika saa 12 zinafungwa, ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya usalama, nataka IGP aniambie kama majambazi ndio wanaotupatia amri...Hatuwezi kukubali kupewa amri na majambazi ni masaa mangapi tunatakiwa kuganya shughuli za kiuchumi au kupangiwa maeneo ya kwenda na wapi tusiende," Waziri Lugola.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushauri kwa mh Lugora :
    Literature inaonyesha nchini UK moja ya mikakati iliyotumika kupunguza uhalifu ni kufanya proactive intervention ikiwemo kuweka taa barabarani. Uhalifu una uwezekano mkubwa kutokea katika mazingira ya giza. Pia structure za nyumba raia waishipo zina mchango mkubwa katika kuendeleza uhalifu. Hivyo km uchumi utaruhusu lifanyie review hilo. Mfano, angalia maeneo hapo dar ambayo mitaa yake ipo rafu na hakuna taa na ulinganishe na maeneo ambayo yako well structured na taa zipo uone utofauti wake katika ujambazi na uhalifu. Muungano wa Pro active intervention na nguvu ya police vitasaidia kupunguza uhalifu. Huko Chicago pia uhalifu, kulingana na literature ulizidi mno na kisa ilisemwa in ni structure ya mji na makazi

    ReplyDelete
  2. Structure itakapokaa vizuri hata ufungaji wa cctv utafanikisha zaidi surveillance

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad