Madiwani Watatu Chadema Watimuliwa Baada ya Kukubali Mwaliko wa Dr. Tulia

Madiwani Watatu Chadema wwwWajiuzulu Nyadhifa Zao
IKIWA ni saa chache baada ya Uongozi wa Chadema mkoani Mbeya kupendekeza kuwavua uanachama madiwani watatu wa chama hicho mkoani humo kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha, madiwani hao wamejiuzulu nyadhifa zao hizo.
Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi).
Madiwani hao wamejiuzulu leo Jumamosi  Julai 21, 2018 baada ya Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu kutangaza uamuzi huo  katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa  vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo.
Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili  hatua zichukuliwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad