Ambapo Upande wa mahakama umedai kuwa Hoja za upande wa utetezi hazina mashiko, chini ya kifungu kilichowasilishwa na upande wa tetezi, ambapo mahakama hiyo imedai kifungu hiko hakipo, mahakama kuu haina uwezo wa kusikiliza kesi iyo, na kutupilia mbali kesi hiyo na kuendelea kusikilizwa tarehe 25 mwezi huu katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Mwenyekiti wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe wanakabiliwa na mashtaka mbali mbali pamoja na wenzake ambayo yalisababisha uharibifu na kifo cha mwanafunzi akwillina mnamo mwezi wa pili mwaka huu 2018.
Pia Bulaya na wenzake wanakabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria Februari 16, katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam; kutotekeleza agizo la polisi lililowataka kutawanyika na kusababisha kifo cha Akwilina Akwilini, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kujeruhiwa askari wawili. Bulaya ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na shtaka la peke yake akidaiwa kushawishi kutendeka kosa la jinai.
Washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa; Naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu; N aibu katibu mkuu (Bara) na mbunge wa Kibamba, John Mnyika; mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.