Mahakama Uganda imeondoa ukomo wa umri kwa Wagombea Urais

Leo July 27, 2018 Mahakama nchini Uganda imehalalisha sheria inayoondoa ukomo wa umri kwa Rais wa taifa hilo, hatua ambayo itamuwezesha Rais Yoweri Museveni kuendelea kugombea katika chaguzi zijazo nchini humo.

Sheria ya Uganda ilihitaji mtu ambaye anagombea urais awe na umri wa chini ya miaka 75 ambapo Rais Museveni anayeongoza Taifa hilo tangu mwaka 1986 asingeweza kugombea tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2021.

Muswada wa kuondoa ukomo wa umri wa mgombea urais uliwasilishwa Bungeni mwezi September na kupitishwa kuwa sheria December 2017, hivyo kusababisha maandamano na shutuma kwa Rais Museveni kutoka kwa Wapinzani.

Kundi la Viongozi wa vyama upinzani vilienda mahakamani kupinga sheria hiyo na kuitaka mahakama kupitia tena sheria hiyo.

Hata hivyo, kundi la Majaji katika Mahakama ya Mbale, Magharibi mwa Jiji la Kampala waliipitisha sheria hiyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad