Maisha yamefanya ngumi kupungua mitaani...

Miaka ya nyuma 2005 kurudi nyuma ilikuwa kawaida kukuta mitaani wanaume/Wanawake wanapigana ngumi kisha wote wanatoana michuzi (damu) kisha maisha yanasonga.
Ni tabia mbovu, lkn siku hizi tabia hii mbovu imepungua kiasi.

Nawaza kwa nini...
1: Hali za maisha zimesababisha watu kujiepusha na maugomvi yasiyo na ulazima.

2: Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa mengi hivyo mtu kufa kwa hata ngumi moja ni jambo la kawaida siku hizi kuliko zamani.

3:Kwa leo tu, ktk pitapita zangu nimeshuhudia gomvi kama nne. mwanamama akigombana na mwenzake kisa siti ya daladala. lkn pamoja na yote gomvi hizo ziliishia katika viwango vya kutishiana, maneno mengi sana, na nusu vitendo lakn hakuna aliyerusha ngumi kwa mwenzake.

4: Tanzania tumekuwa kama familia. Unaweza ukadhani unagombana utaamuliwa, jamaa wasiamue wakakuchukua Video ndani ya Muda mfupi ukawa maarufu kwa ndugu na jamaa nchi nzima kupotia whatsapp,JF, na hata Taarifa ya Habari ( mfano: wale jamaa wa kimara waliokuwa wanagombania urithi).

5:Watu wengi hawali wakashiba achilia mbali wanakula scraps/junk foods hivyo uwezo wa kutawanya nguvu hafifu katika mambo ya ugomvi na kupambana na maisha umekuwa hafifu.


Usipende Kugombanagombana.
Unaweza Ukafa, Ukaua, Ukapata umaarufu hasi nchi nzima ndani ya sekunde, ukaachwa ugombane hadi mwisho bila kuamuliwa maana watu siku hizi hawajali

Top Post Ad

Below Post Ad