Maiti Yakutwa Ikipumua Mochwari

Maiti Yakutwa Ikipumua Mochwari
Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini aliyedaiwa kupoteza maisha zaidi ya siku sita amegundulika kuwa hai, baada ya kuhisiwa anapumua ndani ya Jokofu kwenye chumba cha kuifadhi maiti.

Mkuu wa kitengo cha upasuaji wa hospitali hiyo Gerrit Bradrick amethibitsha kutokea kwa tukio hilo ambapo, mwanamke huyo alipelekwa hospitalini hapo akiwa ameshapoteza uhai baada ya kupata ajali ya gari, lakini cha kushangaza alikutwa akiwa anapumua katika chumba cha kuhifadhia maiti.

“ Mwanamke huyo ambaye hatujamtambua kwa jina lake maana aliletwa na gari la wagonjwa (ambulance) na ilioneonekana kashapoteza maisha lakini, hiyo jana mlinzi wa chumba cha kuifadhi maiti wakati akitekeleza majukumu yake ya alipita kuangalia mwili wa mwanamke huyo katika jokofu na kukuta akipumua”, amesema Dkt. Gerrit Bradrick.

Aidha Dkt. Bradrick hiyo kuwa tukio kama hilo halijawahi tokea, maana kuna tetesi zikidai kwamba wafanyakazi wake walifanya vipimo ambavyo siyo sahihi, na hawana mafunzo ya kutosha jambo ambalo halina ukweli wowote.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad