Makonda Amwagiwa 'Mijisifa'


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo amemwaga sifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa jitiada binafsi za kuwaboreshea walimu mazingira ya kazi ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za walimu.


Waziri Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uzinduzi wa pikipiki 2,894 zenye thamani ya zaidi ya shilling billion 8.5 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu kata ambapo kitaifa zoezi hilo limefanyika Jijini Dar es salaam.

Aidha, Makonda amesema anajivunia kuona Dar es salaam inaendelea kushika kidedea kwenye matokeo ya mitihani ya kitafa kutokana na walimu kuwekewa mazingira bora ya kazi ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za kisasa za walimu, mikopo ya viwanja vya bei nafuu pamoja na kusafiri bure kwenye daladala na treni huku akidai bado ipo mipango mingi ya kuhakikisha walimu wake wanaishi vizuri ili wawe na motisha ya kazi.



Walimu wa Elimu Prof. Ndalichako (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI),  Suleiman Jaffo (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (Kulia) wakiwa wapo juu ya Pikipiki wakizijaribu.

Vile vile, RC Makonda amesema pikipiki zilizotolewa zitaenda kuongeza nguvu na hari ya kazi kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam umepata pikipiki kwa kila Kata.

Pikipiki 2,894 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu Kata nchi nzima zimenunuliwa na Wizara ya Elimu na wafadhili kutoka Global Partnership in education kwa lengo la kuwawezesha kuzitembelea shule kwenye Kata zao ili kuboresha elimu.

EATV

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad