Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, leo Juni 30, 2018, Malima amesema kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa Usalama wa Taifa walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao ambapo muda mchache wenzao wawili walishuka kwenye gari hilo kwa lengo la kukagua gari walilokuwa wakilitumia, ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo.
“Maofisa wawili walishuka kwenye gari, Zacharia alitoka kwake na kukasikika milio ya risasi. Baadaye ilionekana wale maofisa wawili walikuwa wamejeruhiwa kwa risasi. Hivyo waliobaki kwenye gari waliamua kumdhibiti Zacharia na kumtia nguvuni,” amesema Malima.