Mama wa Miaka 91 Amuua kwa Kumpiga Risasi Mwanaye Kuepuka Kupelekwa Nyumba ya Kulea Wazee

Mama wa Miaka 91 Amuua kwa Kumpiga Risasi Mwanaye Kuepuka Kupelekwa  Nyumba ya Kulea Wazee
Mwanamke mwenye umri wa miaka 92 amemuua kwa kumpiga risasi mtoto wake, 72 ili kuepuka kupelekwa kwenye nyumba ya kulea wazee

Anna Mae Blessing, ambaye anashtakiwa kwa mauaji, aligundua nia ya kijana wake kumpeleka kwenye nyumba hiyo, kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani.

''Uliyachukua maisha yangu, hivyo nayachukua ya kwako,'' aliripotiwa akiyasema hayo alipokuwa akisindikizwa kutoka kwenye makazi aliyokuwa akiishi na mwanae na mpenzi wa mwanae

Tukio lilitokea asubuhi ya Tarehe 2 mwezi Julai katika mji wa Fountain Hills nchini Marekani, taarifa ya polisi ilitolewa na vyombo vya habari mjini humo.

Kijana wa Bibi Blessing ambaye jina lake halikuwekwa wazi, alimtaka mama huyo kwenda kwenye nyumba hiyo ya malezi kwa kile alichodai ''imekuwa ngumu kuishi naye''.

Mama huyo alificha silaha zake mbili kwenye mifuko ya koti lake refu kabla ya kumkabili mwanaye aliyekuwa kwenye chumba cha kulala. Taarifa ya polisi ilieleza.


Polisi wamesema walimkuta kijana amefariki na kukuwa na majeraha mawili ya risasi kwenye shingo na taya.

Bibi Blessing alimgeukia mpenzi wa mwanaye mwenye umri wa miaka 57, ambaye alipambana naye na kufanikiwa kumpokonya silaha na kuirusha kwenye kona ya chumba.

Alitoa pisto ya pili, ambayo aliwaambia polisi kuwa alipewa na marehemu mumewe miaka ya 1970.

Mpenzi wa mwanawe alifanikiwa kumpokonya kwa kuupiga mkono wake, kabla ya kutoroka na kuwapigia simu polisi

Polisi walimkuta mtuhumiwa akiwa amekaa kwenye kiti chumbani kwake.Baadae aliwaambia kuwa alistahili ''kuuawa'' kutokana na vitendo vyake.

Bibi huyo amekutwa na hatia ya mauaji, kudhuru mwili na utekaji nyara, na dhamana yake ni kiasi cha dola za marekani 500,000.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad