MAMBO ni hivi! Familia ya staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imesusia mwaliko wa bethidei wa mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye ni mzazi mwenza na msanii huyo.
Familia hiyo inadaiwa kususia mwaliko huo ambao ni wa bethidei ya mtoto wa Mobeto, Abdul Nasibu ‘Dylan’ aliyezaa na Diamond lakini imekuwa bize zaidi na maandalizi ya sherehe ya bethidei ya Tiffah aliyezaa na mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari’ anayeishi nchini Afrika Kusini.
Shamrashamra za sherehe ya Tiffah zimekuwa gumzo kwa takriban majuma matatu sasa, huku familia ya Diamond ikieleza wazi kuwa inajipanga kwenda Afrika Kusini kushiriki kikamilifu.
Chanzo makini kilieleza kwamba familia ya Diamond imegomea kwenda kwenye bethidei inayoandaliwa na Mobeto kwa ajili ya Dylan ambaye pia ni mtoto wa mwanamuziki huyo inayotarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu.
“Unaambiwa familia ya Diamond haitaki kusikia mtu anayeitwa Mobeto maana hawampendi hivyo licha ya kwamba Dylan amezaliwa mwezi mmoja na Tiffah lakini wao wako upande mmoja wa Tiffah,”kilieleza chanzo.