Maneno ya Nape Nnauye Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa

Maneno ya Nape Nnauye Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa
Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Rais Magufuli kutangaza kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Nape amesema anamkaribisha Nchemba kwenye maisha ya kawaida ya ubunge ili kuanza majukumu yake ya kawaida ya kuwatumikia wananchi wake waliompa kura.

“Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!“ameandika Nape Nnaute kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mhe. Nape ni moja ya wabunge wa CCM waliowahi kuteuliwa na kutumbuliwa na Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha mwaka 2015 hadi 2017.

Top Post Ad

Below Post Ad