Mwanadada mwanahrakati katika mitandao ya kijamii mwenye asili ya Tanzania lakini anayeishi Marekani, Mange Kimambi ameshutumiwa na watu wa page mbalimbali za udaku baada ya akaunti ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam kuibwa na watu wasiojulikana na kuvuta kila kitu katika akaunti hiyo.
Mwanadada huyo ambae hapo awali alishutumiwa kuiba akaunti ya Wema sepetu na baada kurudishwa ameingizwa katika swala hilo tena baada ya kuona kuwa aliyeiba akaunti hiyo kufuta na kuwaun-follow watu wote na kuacha jina la mange kimambi tu kama mtu anayemfuata .
Hata hivyo mwanadada huyoa ambae amekuwa akivumbua siri nyingi sana za huku tanzania na pia kusaidia watu wengi kupitia ukurasa wake hajazungumza chochote kama ambavyo imekuwa ikizoeleka kwamba kinapotea kitu kuhusu yeye uongea katika ukurasa wake.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanadada huyo kuambaiwa amefanya vit vya kuumiza mtu mmoja au mwingine tena hasa kwa upande wa Mkuu wa Mkoa hasa kwa sababu hakuna maelewano mazuri kati ya mwanadada huyo na Mh Mkuu wa Mkoa.