Mange Kimambi Amtolea Uvivu Casto Dickson "Hana Faida Yoyote Mariooo Hata Laki Mfukoni Hana"

Mange Kimambi Amtolea Uvivu Casto Dickson "Hana faida yoyote Yeye Mwenyewe Mariooo Hata Laki Mfukoni Hana"
Mwanadada mwanaharakati Mange Kimambi amemtolea uvivu na kumpa makavu yake Casto Dickson ambaye ameonekana akila bata na mpenzi wake Tunda huku mwanaye akiwa kwenye hali mbaya bila yeye kuonekana kuguswa na tatizo alilonalo mwanaye.

Kupitia mtandao wa instagram wa mange kimambi alianza kwa kumtolea uvivu casto kwa kumpa makavu na kuwataka watanzania wasipoteze muda kumtukana tu kwani mwanaume huyo hata laki mfukoni hana na kuwashawishi watoe michango kwaajili ya matibabu.

 Mange aliandika hivi " Ila watanzania tunapenda kupoteza muda na vitu ambavyo havina maslahi kwetu, hiyo nguvu mnayoitumia kumchamba Tunda na Bwanawake si muitumie kumchangia mtoto apate matibabu.....  hivi huyo kaka mnayemchamba eti akamuone mtoto anafaida gani
 hata akienda? Hivi huyu hata laki anayo mfukoni? si ataenda kujaza listi ya wageni tu huko hospitali, mtoto mwenyewe yupo kwenye coma sio kwamba hata yuko macho anamtaka babaake.... Ebu changeni Embu changeni pesa bwana acheni kupoteza mida na upumbavu. Mnamfatilia baba wa mtoto utasema ni mtu wa maana kwamba kuna Msaada anaweza kutoa. Haki ingekuwa labda ni Ruge, Dai, Majey sijui mkaka gani mwingine mwenye maisha yake mazuri haki ningesaidia kumchamba moaka atoe msaada ila huyu mariyooooo mnamchamba ili iweje?? Huyu kaka ni style za kina Petit wanaume suruali, elfu 10 mfukoni hana. Alafu Tunda mnamchamba yeye ndo mwenye mtoto? Au kamfunga kamba huyo Mariyoooo asiende? Na inawezekana huyo kaka hana hata nauli ya kwenda huko Nairobi. Labda mumchangie nauli na malazi🙄, au mlitaka Tunda ndo amlipie nauli na pocket money ampe? Mnampigia kelele baba mtu akamuone mtoto Nairobi wakati mtoto alilazwa Agha Khan wiki 3 na hakwenda kumuona. Hata senti moja ya matibabu hapo Agha Khan hakutoa leo ndio atatoa za Nairobi? Vitu vingine muwage mnajiongeza bwana. Embu tumchangie mtoto acheni kupoteza muda na watu ambao hawana faida yoyote na uponyaji wa huyo mtoto.  "



Top Post Ad

Below Post Ad