Maradona Awatolea uvivu Argentina, Amfananisha Mbappe na Mchezaji huyu Mkongwe Duniani


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona amesema kuwa timu hiyo ya taifa kwa sasa haina maelewano uwanjani kwani wachezaji hawajui cha kufanya pale wanapopata mpira.

Maradona akiongea mapema leo na shirika la Habari la  teleSUR, amesema kuwa safu ya ulinzi ya Argentina imekuwa haina maelewano kabisa na hawajui cha kufanya pale walipokuwa wanapoteza mpira.

“Nimeona timu mbovu kabisa kuanzia ushambuliaji na viungo ukiachana na safu ya ulinzi ambayo naweza kusema imekuwa tenga linalozuia maji, kwani nimeona wote wakipanda lakini linapokuja suala la kuzuia wanafeli, mbele wanamuangalia mtu mmoja hii ni mbaya kwa timu kubwa kama Argentina japo lawama lazima apewe Sampaoli,“amesema Maradona.

Kwa upande mwingine Mshindi huyo wa kombe la dunia la mwaka 1986 amemfananisha mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappé na mshambuliaji mwiba wa zamani wa Argentina, Claudio Paul Caniggia kwa spidi yake uwanjani.

“Nashangaa mabeki wa Argentina dhidi ya timu bora ya Ufaransa yaani kama hawajawahi kumuona Mbappe na wakajisahau wote wakawa wanapanda mbele huku wakimuachia nafasi mtu ambaye ni sura halisi ya Caniggia tena akiwa bado mdogo, wakijua hata mbio hawawezi, kusema ukweli nimeona mpira mbovu kuwahi kutokea katika historia ya timu yangu ya taifa.“amesema Maradona.

Timu ya taifa ya Argentina jana imetolewa kwenye michuano ya kombe la dunia kwa kipigo cha goli 4-3 dhidi ya Ufaransa.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad