Mbwana Samatta Kucheza Ligi Moja na Messi

Jina la nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ameanza kuzivutia club za Ligi Kuu Hispania na hiyo imeripotiwa na mtandao wa macholevante.com kuwa wanamuhitaji

Mbwana Samatta ameripotiwa na macholevante.com kuhitajika na club ya Levante ya Hispania ambayo itashiriki Ligi Kuu Hispania msimu wa 2018/19, Levante imeonesha jitihada za kutaka kumsajili Samatta kufuatia kuumia kwa mshambuliaji wao Emmanuel Boateng.

Levante wametenga kiasi cha euro milioni 4 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 10.6 ili kunasa saini ya Samatta ambaye pia inaripotiwa kuna timu ya Ligi Kuu Ujerumani Bundeslinga inamtaka staa huyo, kama Samatta atajiunga na Levante atakuwa kapata nafasi ya kwenda kucheza Ligi moja na Lionel Messi wa FC Barcelona.

Mbwana Samatta ambaye alijiunga na KRC Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe kwa ada ya uhamisho wa euro laki 8, hadi sasa ameichezea Genk jumla ya mechi 54 na kuifungia magoli 17 na magoli mawili katika michuano ya UEFA Europa League.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad