Mengi Azindua Kitabu Chake Asimulia Maisha Magumu Aliyopitia " Nililala Chini Wageni Wangu Walikuwa Mende na Panya"

Mengi Azindua Kitabu Chake Asimulia Maisha Magumu Aliyopitia " Nililala Chini Wageni Wangu Walikuwa Mende na Panya"
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi leo Jumatatu Julai 2, 2018 amezindua kitabu chake kiitwacho ‘I can, I must, I will’ chenye kurasa 311, katika hafla iliyofanyika jijini hapa na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli.

Kitabu hicho kina ujumbe mbalimbali kuhusu masuala ya kitaifa, kiroho, mafanikio na mafunzo mbalimbali kwa vijana hasa katika ujasiriamali na kujitegemea.

Akizungumzia kitabu hicho, Dk Mengi amesema kimeelezea maisha yake kabla ya mafanikio na mambo aliyoyafanya baada ya kupata mafanikio.

“Maisha yangu awali nililala chini wageni wangu walikuwa mende na panya lakini niliamua kuwa ninaweza kuondoka kwenye umaskini na niliamua kuondoka katika hali hiyo na niliweza kweli,” amesema Mengi.

Amesema wazazi wake walikuwa masikini lakini wenye uwezo wa kujituma katika kazi.

“Mama yangu aliitwa mama wa kibiashara, baba yangu alikuwa ananunua kondoo waliokonda sana anawalisha na baada ya kuuza anauza kwa bei kubwa,” amesema.

Amesema baadhi ya watu humhoji kwamba anasaidia watu na anaweza kufilisika, “nina wajibu hata nikiishi miaka mia sitafilisika, siogopi, Mungu alinifundisha kutoa, mama yangu chakula aliwapa watoto wasioweza, wale ndio sisi tulikula kwa hiyo nimejifunza mbali hili.”
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad