Meya Awaajili Warembo Katika Kitengo cha Usalama Barabarani Huku Akiwataka Wavae Nguo Fupi

Meya Awaajili Warembo Katika Kitengo cha Usalama Barabarani Huku Akiwataka Wavae Nguo FupiMeya wa mji wa Broummana nchini Lebanon Pierre Achkar amewaajili warembo wa vyuo vikuu katika kitengo cha maafisa usalama barabarani huku akiwapa mashariti ya kuzingatia.


Mabinti wa vyuo waliojiliwa na Jeshi la Polisi nchini Lebanon.

Pierre ametoa nafasi hiyo kwa mabinti wa vyuo vikuu kuajiliwa ili kufanya kazi na maafisa usalama barabarani huku akiwataka kuvaa nguo fupi kwa kile alichodai kuwa ni sehemu ya kuvutia vyombo vya habari, ndani na nje ya nchi.

"Sababu kubwa ya kuajili mabinti hawa ni kuongeza mvuto katika maeneo yetu ya mji na kuvutia vyombo vya habari ambapo tutapata namba kubwa ya watalii na kukuza uchumi wa nchi yetu”, amesema Pierre.

Hili ni agizo la pili kutoka kwa Pierre baada ya siku chache zilizopita kutoa agizo kwa walimu wa mazoezi ya viungo kufundisha mabinti pembezoni mwa barabara mjini Broummana ili kuwavutia watalii.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad