Mfanyabiashara maarufu wilayani Musoma, Peter Zakaria, amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mawili ya kujaribu kuua.
Zacharia amesomewa mashtaka hayo leo Julai 5, mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Rahimu Mushi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, akidaiwa kuwapiga risasi Ahmed Segule na Isaac Bwire ambao hata hivyo hawakutajwa ni wakazi wa wapi wala kazi yao.
Baada ya kusoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Lukelo Samuel aliiomba Mahakama kuzuia dhamana ya mshtakiwa kwa sababu hali ya waliojeruhiwa bado ni mbaya na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Maombi hayo yalipingwa na Mawakili wa mshtakiwa Kassim Gile na Onyango Otieno wakisema hayana msingi na kwamba dhamana ni haki ya mshtakiwa na shtaka linalomkabili linadhaminika.
Baada ya kusikiliza hoja za zote mbili, Hakimu Mushi ameahirisha shauri hilo hadi Julai 10 atakapotoa uamuzi wa kutoa au kuzuia dhamana. Mshatakiwa amepelekwa mahabusu kusubiri uamuzi wa mahaka
Juni 30, Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima aliwaambia waandishi wa habari kuwa waliojeruhiwa katika tukio hilo lililotokea mjini Tarime saa 2 usiku wa Juni 29 ni Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa waliofika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa ajili ya kujaza mafuta kwenye gari lao.
Mfanyabiashara Peter Zakaria Afikishwa Mahakamani Kwa Kutaka Kuua Anyimwa Dhamana
July 05, 2018
Tags