Mfanyakazi (Msaidizi wa Nyumbani) Ana Busara Kuliko Mke Wangu

Wandugu, mimi ni mfanyakazi wa Benki mmojawapo hapa Dar es Salaam,
1. Nimeoa mwaka wa 7 sasa, nina watoto watatu, wawili kati yao wanasoma Shule ya Msingi.

2. Dada wa kazi hapa nyumbani (Housegirl) tupo nae mwaka wa 5 sasa. Kiukweli (bila unafiki) Dada huyu ni mtu mwenye busara na mvumilivu pia mchapakazi haswaa na anawajali watoto katika kuwaandaa kwenda shule, usafi wa nyumbani, vyakula (pia kubana matumiz yasiyo ya lazima).

3. Mke wangu naye ni mfanyakazi (Mwalimu wa Shule ya Msingi, tatizo lipo kwenye namna tunavyoishi humu ndani, mke amegeuka kuwa mtu wa KUGOMBEZA, akiingia home anagombezwa kila mtu kuanzia House girl, mimi mumewe na changanya watoto.

4. Pamoja na kugombezwa kote huko binti wa kazi huwa hajibu zaidi ya kuwa mkimya kisha huendelea na kazi zake, na wakati mwingine huomba radhi hata kama kosa si lake.

5. In short, mama mwenye nyumba akiwepo ni wote tunakuwa wapole, ni mwendo wa kugombezwa tu mpaka inapofika mida ya kulala, takribani saa 5 usiku.

NB: Najuta kumuoa huyu mwanamke wa Kichaga toka Lambo, Machame.

Blessings/JF
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad