NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali toka Wizara hiyo.
Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo ilianza juzi wilayani Handeni.
Alisema mradi huo ulitakiwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali .
Akiwa kwenye mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora mrai huo.
“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akizungumza na Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Joseph Mcharo kabla ya kumsimamisha kazi kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe