Missy Elliott Amfanyia Surprise hii Iggy Azalea

Missy Elliott amfanyia surprise hii Iggy Azalea
Iggy Azalea humuelezi kitu kwa rapper Missy Elliott. Mrembo huyuo alipata mshangao mkubwa wiki hii baada ya kupokea simu kutoka kwa rapper huyo ambaye amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu..

Iggy alipokea simu hiyo wakati alipokuwa kwenye kipindi cha The Cruz Show ya Power 106’s na kuthibitisha kuwa Missy Elliott ndio role model wake.

"Nahisi kama kufa kweli hivi sasa. Ninakupenda, wewe ni shujaa wangu. Wewe ni shujaa wangu kabisa wa maisha.



Azalea aliongeza kuwa video ya ngoma ya One Minute Man ya Missy Elliott ambayo imetoka zaidi ya miaka tisa iliyopita ni miongoni mwa video zake tatu bora za  muda wote kutokana na ubunifu uliotumika ndani yake.

Hata hivyo Elliott amempongeza Iggy kwa kazi yake anayofanya kwenye muziki, "Endelea kufanya jambo lako. Hongera juu ya mafanikio yako yote!."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad