Kiungo Mkongomani aliyetua Simba kwa ajili ya kufanya majaribio, Fabrice Kakule, amerejea Rwanda kwa ajili ya kumalizana na uongozi wa Kiyovu SC.
Kakule aliwasili nchini kwa ajili ya kupiwa kiwango chake lakini baadaye kukaibuka taarifa kutoka kwa mabosi wake wa Kiyovu wakieleza kuw bado ana mkataba.
Kutokana na Kiyovu kuja juu huku wakiipa onyo kali Simba, mchezaji huyo imebidi arejeshwe ili kuweka mambo sawa ambapo sasa atapaswa kwenda kumalizana viongozi wake na mambo yakiwa mazuri atarudi kujiunga Simba.
Kakule aliwasili hapa nchini akipendekezwa na Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma ili kuja kufanyiwa majaribuo kwa lengo la kuipa nguvu safu ya kiungo endapo atafuzu kisha kupewa mkataba.
Wakati Kakule akirejea Rwanda, kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na siku chache zijazo kitasafiri kuelekea Uturuki kwa kambi ya wiki mbili.