Watanzania wametakiwa kumuunga mkono rais John Magufuli kwa juhudi anazofanya kuimarisha uchumi na kuwahudumia wanyonge wenye shida bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.
Mwenyekiti wa taifa wa bodi ya Parole, Agustine Mrema amesema hayo wakati wa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kupona maradhi ya saratani kwenye parokia la Uomboi ya kanisa katoliki jimbo kuu Moshi.
Mrema amesema kuwa tangu aingie madarakani rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuwasaidia watu wenye matatizo ikiwemo yeye kwa kumpeleka India kupata matibabu na katika hali hiyo alianzisha mchango kanisani wa ujenzi wa nyumba za mapadre wa parokia ya Uomboi kama sadaka ya kumshukuru mungu.
Akizungumza baada ya ibada hiyo paroko wa parokia ya Uomboi Padre Juvenal Kimario amemshukuru Dkt.Mrema kwa kuanzisha mchango huo ambao zitahitajika shs.28mil/= kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo iliyokwenda sanjari na uzinduzi wa uzinduzi wa serikali ya kijiji cha Kiraracha wamewataka viongozi wengine kuiga mfano wa kumshukuru mungu hadharani baada ya kupata shida mbali mbali.