Mrembo Demi Lovato alazwa ghafla hospitalini, yadaiwa amezidiwa na madawa ya kulevya


Muigizaji na mwanamuziki kutoka nchini Marekani Demi Lovato usiku wa kuamkia leo Jumatano Julai 25, 2018 amelazwa hospitalini ghafla  baada ya kuzidiwa na Madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Demi Lovato (25) aliwahishwa hospitali mjini Los Angeles baada ya kikosi cha Polisi mjini humo kupata taarifa ya dharura ya uhitaji wa msaada wa haraka wa matibabu ‘Medical Emergency’ kutoka kwa watu wa karibu wa msanii huyo.

Lovato miaka miwili iliyopita alibainika kuwa na matatizo ya kiakili yaliyosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo baadae akiwa kwenye sober house alikimbia matibabu hayo.

Msanii huyo mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana nchini Marekani aliushangaza ulimwengu mapema mwaka huu baada ya kuachia wimbo wa SOBER ambao kwenye moja ya mashairi yake alisikika akisema kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya.

Hata hivyo bado taarifa za kitibabu hazijatoka kama kweli mrembo huyo jana alizidiwa na madawa ya kulevya au laah! .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad