Mrembo Pretty Kindy Adaiwa Kula Makombo ya Wema Sepetu

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ anadaiwa kula makom­bo ya msanii mwenzake, Wema Sepetu kwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo aliyewa­hi kubanjuka penzini na Wema, Calisah Abdul­hameed.

Kikizungumza na Za Mo­tomoto News, chanzo ma­kini kilieleza kuwa Pretty Kind amekuwa akioneka­na mara kwa mara maeneo ya Sinza, Dar akiwa na Calisah wakionyeshana mahaba niue hivyo ndiye mtu wake kwa sasa.

Za Motomoto News ilimtafuta Pretty Kind akafunguka:“Siyo kweli tupo karibu na Calisah kwa sababu ya kazi na siku ikimalizika mashabiki wataiona.”

Top Post Ad

Below Post Ad