MKURUGENZI wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Hassan Abbas, leo ameongea na wanahabari jijini Dodoma jinsi serikali ya awamu ya tano inavyoendelea kutekeleza kwa kasi ahadi zake.
Alisema hadi kufika machi 2017, pato la taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016 na kwamba serikali imetimiza ndoto ya kuendelea kulifufua shirika la ndege nchini (ATCL) kwa kuleta ndegeaina ya Boeing 878 Dreamliner, ambapo ndege nyingine mbili za C Series zinakuja Novemba na Boeing nyingine moja itakayowasili Januari 2020.
“Tangu ujio wa ndege hizi abiria wa ATCL wameongezeka hadi kufikia 107,207 katika mwaka 2016/2017 kutoka 49,174 mwaka 2015/2016 pia serikali imeendelea kutekeleza agizo la serikali kuhamia Dodoma ambapo takribani watumishi 6,400 wameshahamia,” alisema.