Msigwa afichua jinsi CCM walivyomuibia wazo lake

Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA), amedai kuwa yeye ndio alikuwa wa kwanza kutoa kauli ya kupeleka runinga katika soko la Mlandenge lakini Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilimuwahi kwa kupeleka kabla yake.

Akizungumza kupitia East Africa BreakFast ya East Africa Radio, Msigwa amesema kwamba, yeye alikuwa wa kwanza kutoa ahadi lakini CCM walimuwahi na kupeleka kabla yake hivyo anawashangaa wananchi wanaombeza juu ya jambo hilo bila ya kujua undani wake.

“CCM waliniwahi kupeleka televisheni hiyo hapo sokoni na wananchi wanaohoji kuhusu suala hilo basi wakitaka nilete televisheni nyingine na zifungwe mbili katika soko sawa nitafanya ivyo”, amesema Msigwa.

Aidha Msigwa ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana wafadhili kutoka benki ya dunia watakamilisha mradi wa soko la ghorofa ili kuboresha huduma sokoni hapo na kulifanya la kisasa.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad