Mtibwa Yatakiwa Kupeleka Haraka Vithibitisho TFF vya Malipo ya CAF

Mtibwa Yatakiwa Kupeleka Haraka Vithibitisho vya Malipo ya CAF
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), limeibana klabu ya Mtibwa Sugar juu ya malipo ya deni lao la faini katika Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa kuwataka wapeleke uthibitisho ili wapate nafasi ya ushiriki Kombe la Shirikisho baadaye mwaka huu.

Awali kulikuwa na sinto­fahamu juu ya ushiriki wa Mtibwa Sugar katika michua­no ya Kombe la Shirikisho mwaka huu hadi TFF ilipopa­ta ufafanuzi Caf ambapo imeitaka klabu hiyo kulipa kiasi cha dola 15,000 ndio washiriki.

Mwaka 2003, Mtibwa Sugar ilifungiwa na CAF miaka mitatu kutoshiriki michuano yoyote inayosimamiwa na shirikisho hilo kutokana na kushindwa kwenda kucheza dhidi ya Santos FC ya Afrika Kusini, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kile kilichodaiwa kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikosa fedha za nauli za kuisafirisha timu.

Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo hapa nchini Mtibwa Sugar ilikubali kipigo cha mabao 3-0. Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa iwapo Mtibwa wamelipa fedha hizo.

“Mtibwa kama wao wa­nasema wamelipa fedha hizo wanazodaiwa basi ni vyema wakaleta uthibitisho TFF ili waweze kupata nafasi ya kushiriki,” alisema Karia.

Mara ya kwanza kwa Mti­bwa Sugar kushiriki michuano hiyo ilikuwa mwaka, 2001, kisha ikashiriki 2002 na mara ya mwisho ilikuwa ni 2003.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad