Mtoto wa Darasa la kwanza [jina tunalihifadhi] mwenye umri wa miaka nane (8) mwanafunzi wa shule ya Msingi Maganjwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Babati amefanyiwa kitendo cha ubakaji akiwa anaenda mashine kusaga unga wa ugali hali iliyomsababishia maumivu makali na kuwalazimu madaktari kumfanyia upasuaji.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Maganjwa Petro Shauri alisema majira ya jioni mtoto huyo alitumwa mashineni kusaga mahindi kwa ajili ya chakula cha nyumbani na alipofika msagaji alimwagiza arudi nyumbani kuchukua hela kwani alifika mashineni hapo akiwa hana hela na pia walikuwa wakidaiwa.
“Wakati akirejea nyumbani kumpa taarifa mama kwamba wanadaiwa ndipo alipokutana na mwanaume huyo na kufanyiwa kitendo hicho cha ubakaji’,.alisema Mwenyekiti
Aliendelea kusema ‘ilipofika usiku mama akastuka mbona mpaka sasa simwoni mwanangu ndipo aliamua kwenda mashineni kumfuata na alipomuuliza Yule msagaji akamwambia nilishamuagiza muda mrefu aje umpe hela’.mwenyekiti alisimulia
Mwenyekiti alisema Mtuhumiwa alikamatwa usiku huo na kupelekwa katika ofisi ya kijiji hadi asubuhi na kupelekwa kituo kidogo cha polisi Dareda.
Mama mzazi wa mtoto aliefanyiwa kitendo hicho Maria Domisiana amesema akiwa na majirani wakimtafuta alikumkuta mtoto wake akiwa na matope kichwani na alipomuuliza umepatwa na tatizo gani ndipo alipoanzanza kumsimulia kuwa alikutana na Salao akamwambia twende tukachukue ndoo ya mama ana alipokataa akamkamata kwa na kmpeleka katika shamba la shule na kuanza kumvua nguo huku akimng’ata na kasha kumbaka huku akiwa amemziba mdomo.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Dareda Josef Lorry amesema kuwa mtoto huyo amepata ugonjwa wa Fistula kati ya sehemu yake ya haja ndogo na kubwa.
Lorry amesema tukio hilo limemuathiri mtoto huyo kisaikolojia lakini pia athari za kihisia na kimaumbile kwa sababu ya kuharibiwa sehemu zake za siri.
Mtoto huyo kwa sasa yupo katika hospitali ya Wilaya, Dareda akiendelea kupata matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kumrudishia hali yake ya kawaida