Mubenga Afunguka Afya ya Ommy Dimpoz

Mubenga Afunguka Afya ya Ommy Dimpoz
Kama utakuwa ni shabiki wa Ommy Dimpoz basi utakuwa uliwahi kusikia kwenye intro ya nyimbo za zake akitaja jina ‘Mubenga’ basi huyo alikuwa Meneja wake siku za nyuma.

Mubenga amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kwamba hamsimamii Tena Ommy kikazi lakini hana bifu naye ameshampigia kumjulia hali siku nyingi.

Ommy Dimpoz alitangaza siku ya Eid kuwa alikuwa anaumwa sana mpaka kufanyiwa operesheni ya koo na kusema alikuwa hoi kitandani nchini Afrika ya Kusini.

Mubenga alifunguka haya kuhusu afya ya Ommy Dimpoz na uhusiano wao kwa sasa mara baada ya kuacha kufanya kazi pamoja:

Unajua watu wamekuwa wakirushiana Kimitandao sana sio kila kitu lazima tuweke kwenye mitandao.

Nimewasiliana na OMMy na nimempa pole na watu wajue kuwa sisi hatuna ugomvi na hata tatizo lake lilimuanza muda kidogo maana alikuwa hawezi Kula mpaka awe na maji pembeni maana koo lake lilikuwa halipitishi chakula vizuri.

Lakini sasa tunashukuru Mungu tunamuombea apone kabisa na kurejea kazini “.

Ommy Dimpoz hivi sasa yupo chini ya uongozi mpya wa Rockstar 4000 ambao upo chini ya staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad